47 views
1 month ago General
USALAMA MITAANI
Usalama umeimarishwa katika eneo bunge la Hamisi, Kaunti ya Vihiga, kufuatia ushirikiano wa karibu kati ya wakazi na maafisa wa usalama, huku viongozi wa jamii wakiwataka wananchi kuendelea kutoa habari mwafaka kwa maafisa husika ili kutokomeza uhalifu. Wito huo ulitolewa wakati wa uzinduzi wa lango jipya la Kituo cha Polisi cha Cheptulu, lililojengwa kwa hisani ya wakfu wa Rogers Bwosi kama sehemu ya jitihada za kuboresha miundombinu ya kituo hicho na kuimarisha ulinzi wa jamii. Rogers Bwosi, mwasisi wa wakfu huo aliwasifu maafisa wa kituo hicho kwa kujitolea katika utumishi wa umma akisema kuwa usalama unaweza tu kudumishwa kupitia kuaminiana na ushirikiano kati ya polisi na wakazi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive