23 views
1 week ago General
Mazungumzo baina ya baraza la magavana na chama cha wauguzi yamegonga mwamba, hali inayoendeleza mgogoro wa kiafya ulioathiri vituo vya afya ya umma katika kaunti zote humu nchini. Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wauguzi na wakunga Seth Panyako, ametangaza kuwa mgomo huo ulio katika wiki ya tano utaendelea, licha ya kuafikia makubaliano na baraza la magavana kuhusu uajiri wa wafanyakazi wa mpango wa huduma za afya kwa wote kwa masharti ya kudumu. Kutoelewana sasa kumesalia kwenye suala la utekelezaji wa mkataba wa makubaliano.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News