9 views
1 week ago General
Serikali imeondoa mbali wasiwasi kuhusu kuwepo kwa mgogoro katika sekta ya elimu ya juu kuhusiana na mpito wa mfumo mpya wa ufadhili katika vyuo vikuu ambao umechelewesha usambazaji wa fedha kwa wanafunzi. Katibu katika idara ya elimu ya juu Dkt. Beatrice Inyanga amesema wanafunzi zaidi ya elfu 195 wa mwaka wa kwanza tayari wamejiunga na vyuo vikuu huku serikali ikiendelea kutekeleza mpango mpya wa ufadhili. Alisema haya jijini Nairobi leo wakati wa mkutano wa mashauriano na manaibu wa machansela wa vyuo vikuu kuhusu utekelezaji wa mfumo wa kitaifa wa kuhitimu na hifadhi ya kitaifa ya takwimu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive