5 views
1 week ago General
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa kujumuishwa kwenye sheria, kutoweka kwa watu wanaotekwa nyara humu nchini yakisema kutokuwepo kwa sheria bayana kunaifanya iwe vigumu kuwachukulia hatua watu wanaohusika na vitendo hivyo na kuziacha familia za waathiriwa kwenye njia panda. Yakiongea katika kaunti ya Mombasa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya waathiriwa wa utekaji nyara, mashirika hayo pia yametoa wito wa utekelezaji kikamilifu wa sheria ya kuwalinda waathiriwa wa utekaji nyara ya mwaka 2014, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao yakisema visa vya utekaji nyara na kutoweka kwa watu huongezeka wakati wa misimu ya chaguzi. Kulingana na takwimu zilizowasilishwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu, takriban visa 196 vya kutoweka kwa watu vimeripotiwa nchini Kenya tangu mwaka 2019.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive