9 views
1 week ago General
Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichung’wah na mwakilishi wa wanawake bungeni katika kaunti ya Nyandarua Faith Gitau, wametoa wito wa umoja na mazungumzo baina ya wakenya, kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Viongozi hao walioandaa kikao cha umma na viongozi wa mashinani kutoka maeneo ya Kipipiri na Kinangop, kaunti ya Nyandarua, walisema maamuzi ya kisiasa yanafaa kuelekezwa na mahitaji ya wakenya wa kawaida, na haja ya kuunganisha taifa, na wala sio kwa manufaa ya kibinafsi ya wanasiasa. Huku hayo yakjiri, gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na baadhi ya wabunge kutoka kaunti ya Kakamega wamewaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia wahuni na magenge ya wahalifu kutatiza mikutano ya umma.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive