1 views
1 week ago General
Familia moja katika kaunti ya Kiambu inatoa wito kwa wahisani kusaidia katika mchango wa takriban shilingi milioni moja za kumsaidia jamaa wao mwenye umri wa miaka 65, George Njoroge Njuguna ili kupata matibabu ya figo pamoja na kukidhi mahitaji mengine ya dharura. Njuguna amekuwa akikabiliwa na tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi, hali iliyomfanya kufanyiwa matibabu ya figo kwa kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja. Akizungumza na runinga ya KBC Channel One katika hospitali ya Nazareth kaunti ya kiambu ambako amelazwa, familia imesema kufikia sasa, imeshindwa kugharamia matibabu yake.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive