4 views
1 month ago General
Wizara ya afya pamoja na hazina ya Beginnings,zimetia saini makubaliano ya shilingi bilioni kumi kuboresha afya ya akina mama na watoto. Makubaliano hayo ya miaka mitano yanalenga kuimarisha huduma za afya kwa akina mama wajawazito ili kupunguza vifo vya watoto wachanga wakati na baada ya kuzaliwa.Hazina hiyo ya Beginnings itafadhili utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kunufaisha hospitali mia mbili katika kaunti 21 zikiwemo kaunti za Tana River, Garissa, Isiolo, Homa Bay na Kisumu miongoni mwa kaunti nyingine.Waziri wa afya Aden Duale alisema huku hazina hiyo ikitoa usaidizi wa kifedha,serikali itaangazia kuboresha mifumo ya afya iliyoko,kudumisha imani ya umma katika huduma za afya na kuhakikisha miradi hiyo inaendelezwa ipasavyo hata baada ya muda wa ufadhili kukamilika.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive