3 views
1 month ago General
Mbunge wa Teso kaskazini Oku Kaunya amewahimiza wakazi kujiunga na vyama vya mikopo na akiba kama njia moja ya kukabili umaskini na kujiimarisha kiuchumi. Kaunya alisema akiba huwezesha wanachama kupata mikopo ya viwango vya chini vya riba ili kuwekeza kwenye biashara,kuimarisha mapato ya kijamii pamoja na hali ya kiuchumi ya familia zao.Akiongea wakati wa hafla ya kutoa hamasa kwa wanachama iliyoandaliwa na chama cha ushirika cha Ports SACCO katika ukumbi wa chama cha KNUT huko Amagoro,mbunge huyo alisema wakazi wengi wamelazimika kutegemea mikopo yenye viwango vya juu vya riba au misaada ya kifedha kutoka kwa marafiki na jamaa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive