2 views
1 month ago General
Viongozi wa kike wamewarai wadau katika sekta ya usawa wa kijinsia kuongeza jitihada za kuashirikisha zaidi wanawake katika maamuzi muhimu na nafasi za uongozi katika nyanja zote. Wakizungumza wakati wa kikao cha Mpango wa Wanawake Kwenye Uongozi katika Chuo Kikuu cha Nairobi wanachama wa vuguvugu la Women Caucus walisema licha ya hatua zilizopigwa, wanawake bado wanakabiliwa na vizingiti vinavyowazuia kupata fursa za uongozi kwenye siasa, biashara, elimu na huduma kwa umma. Viongozi hao walihimiza mashirika ya serikali, washirika wa maendeleo, sekta ya binafsi na mashirika ya kiraia kushirikiana katika kukuza sera zinazotilia maanani usawa wa kijinsia, kuimarisha mipango ya uwezeshaji na kuwekeza katika kuwakuza wanawake na wasichana.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive