19 views
1 month ago General
Walimu wa Madrasa na Duksi wametoa wito kwa tume ya kuajiri walimu-TSC kuwapa ajira kuambatana na agizo la serikali la kujumuisha mafunzo ya dini ya Kiislamu kwenye mtaala wa elimu. Ujumbe huu ulitolewa wakati wa mafunzo ya siku tatu ya kuimarisha uwezo wa walimu. Wakiongozwa na mdhamini wa Baraka Trust Sheikh Shamy Athman, walimu hao wanataka kutambuliwa kamili na kujumuishwa rasmi katika mfumo wa elimu, wakisema kwamba wanatekeleza jukumu sawa na walimu walioajiriwa na tume ya TSC. Fauka ya hayo wanataka kuajiriwa kupitia njia zilizoanzishwa za kitaalamu ili kufanikisha mpito huo. Mafunzo hayo ya siku tatu yanaendelea katika msikiti wa Al-Huda jijini Nairobi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive