9 views
1 month ago General
Kenya inaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Marekani katika juhudi za kukuza sekta ya utalii na kuvutia uwekezaji zaidi nchini. Ujumbe wa wabunge wanane kutoka Kamati ya Bunge la Marekani inayoshughulikia biashara na kawi umeanza ziara yake nchini kwa mazungumzo na Waziri wa Utalii na Wanyamapori Rebecca Miano kabla ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara. Serikali inasema ziara hiyo ni fursa muhimu ya kuitangaza Kenya kama kitovu cha utalii duniani na kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, uhifadhi wa mazingira na kawi. Wabunge hao wanatarajiwa kushuhudia uhamaji mkubwa wa nyumbu katika eneo la Maasai Mara, huku Kenya ikitarajia kuwa watakuwa mabalozi wa kuitangaza nchi kimataifa kama kivutio cha utalii.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive