19 views
1 month ago General
Familia moja mtaani Embakasi eneo la Muradi inaomba msaada wa kifedha ili kupata mwili wa binti wao ambao umesalia katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta baada ya kushindwa kulipa ada za matibabu za shilingi milioni 2.51. Marehemu Sherry Bahati mwenye umri wa miaka 8 alifariki mapema mwezi huu kutokana na uvimbe kwenye ubongo baada ya upasuaji. Familia yake imeshindwa kuchukua mwili huo ili kwenda kuuzika kutokana na deni la bili ya hospitali. Wanatoa wito kwa wasamaria wema kuwasaidia kulipa gharama hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive