30 views
1 month ago General
Familia moja huko Ruiru kaunti ya Kiambu, inatafuta haki baada ya kushambuliwa na watu waliojihami kwenye barabara ya Ruiru bypass na gari lao kuharibiwa. Jared Onsase ambaye ni dereva wa gari la usafiri wa umma, alikuwa ameegesha gari lake kando ya barabara alipoona gari aina ya Subaru limekwama barabarani. Inadaiwa dereva wa gari hilo alimlazimisha kutoka kwenye gari lake na kujaribu kumpiga risasi. Ugomvi huo uliwavutia wananchi ambao waliwaarifu maafisa wa polisi ambao walifika mahali na kutuliza hali. Magari yaliyohusika kwenye kioja hicho yalizuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive