11 views
1 month ago General
Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt. Raymond Omollo amewataka wakazi wa eneo la Nyanza na taifa nzima kwa ujumla kuunga mkono wito wa Rais Ruto wa kuzinduliwa kwa mazungumzo ya kitaifa mnamo Agosti 12. Akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha katika Shule ya Upili ya Balozi Pamela Mboya huko Homabay, Omollo aliangazia rekodi ya serikali ya Kenya Kwanza katika eneo hilo na kwingineko, akisema wakati umewadia wa mazungumzo ya wadau mbalimbali ili kupanga mpango kamili wa maendeleo ya kitaifa. Omollo pia alitoa wito kwa usimamizi wa shule za upili kuwasajili wanafunzi wenye umri wa miaka 18 na zaidi kupata vitambulisho ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uchaguzi nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive