14 views
1 month ago General
Kenya kwa kushirikiana na mataifa jirani imeimarisha ufuatiliaji wa magonjwa katika maeneo ya mipakani na kubadilishana taarifa kwa wakati halisi ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa hatari katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni, amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha utayari na uwezo wa nchi wanachama kukabiliana kwa pamoja na magonjwa yanayoweza kuzuka kama vile Ebola na Mpox. Muthoni amesema Kenya haijarekodi kisa chochote cha Ebola, huku ufuatiliaji ukiimarishwa katika mipaka yote ya kuingilia nchini kupitia ushirikiano wa kikanda.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive