4 views
1 month ago General
Serikali imeimarisha juhudi za kuwianisha mafunzo ya kitaaluma na mahitaji ya kazi viwandani kupitia ushirikiano mpya utakaowawezesha wanafunzi wa vyuo vya TVET kupata mafunzo ya vitendo na vyeti vya kitaalamu katika tasnia ya upakaji rangi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Nairobi, Katibu katika idara ya elimu ya kiufundi na mafunzo anuwai Esther Muoria, alisema hatua hiyo inalenga kuwandaa waliohitimu kwa ajira, kukuza wajasiriamali na kuziba pengo la ujuzi katika sekta ya ujenzi inayokua kwa kasi nchini Kenya. Mpango huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa mara moja katika taasisi za TVET kote nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News