14 views
1 month ago General
Wizara ya Elimu imejiondolea lawama ya ucheleweshaji wa fedha zinazotolewa kwa shule, taasisi za kiufundi na vyuo vikuu na Hazina ya Kitaifa ikisema mgogoro wa ufadhili wa elimu humu nchini umekiuka madai ya usimamizi mbaya. Waziri wa elimu Julius Ogamba aliyefika mbele ya kamati ya uwekezaji wa umma katika bunge la seneti alisema wizara hiyo imekuwa ikituma maombi ya ufadhili kwa wakati na kisha kusambaza fedha hizo pindi zinapotolewa na hazina kuu. Hata hivyo, kulingana na Ogamba, mgao wa rasilimali kwa sekta hiyo umeshindwa kuwiana na idadi kubwa ya wanafunzi na gharama inayoongezeka ya masomo hivyo kuziacha taasisi za elimu na mzigo wa madeni.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive