2 views
2 months ago General
Wanafunzi wawili wa shule za upili wamefariki huku watu wengine wanne wakijeruhiwa katika ajali tofauti za barabarani zilizotokea katika kaunti za Nairobi na Bungoma. Jijini Nairobi, mwanafunzi mmoja aliyekuwa amebebwa kwenye pikipiki alifariki baada ya lori lililokuwa likisafirisha mchanga kupoteza mwelekeo katika barabara ya Charles Lwanga na kuigonga pikipiki hiyo, kabla ya kuvunja ua la shule na kuingia darasani. Katika kaunti ya Bungoma, eneo la Mayanja, mwanafunzi mwengine alifariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya trela kupoteza mwelekeo na kuwagonga walipokuwa njiani wakielekea shuleni.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive