19 views
2 months ago General
SAKAJA KWENYE RATILI
Mkaguzi mkuu wa hesabu za matumizi ya pesa za serikali alithibitisha kuwa gavana wa Nairobi hasimamii kikamilifu mfumo wa ukusanyaji mapato ya shilingi bilioni-2.7 iliyonunua. Kulingana na afisi ya mkaguzi mkuu, gatuzi hilo liliafikiana na mfanyabiashara wa serikali ya kitaifa bila ya kufuata taratibu zinazofaa kununua mfumo huo. Mkataba huo unamruhusu mfanyabiahara huyo kukusanya asilimia-4.5 ya mapato yaliyokusanywa kugharamia ada za utoaji huduma. Akiwa mbele ya kamati ya bunge la seneti, gavana wa Nairobi Johnstone Sakaja alitakiwa kuelezea kwa nini gatuzi hilo lilitumia shilingi milioni-850 kuzindua chumba cha seva kinachodaiwa kutotumiwa kikamilifu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive