16 views
1 month ago General
Maandalizi ya makala ya sita ya Tamasha ya Piny Luo yameanza huku Kaunti ya Kisumu ikijiandaa kwa hafla hiyo ya kila mwaka. Gavana wa kaunti ya Kisumu Profesa Anyang' Nyong'o alikutana na Baraza la Wazee wa jamii ya Waluo ambapo walifichua kwamba kamati ya kiufundi itaongoza maandalizi ya tamasha hiyo iliyopangwa kuandaliwa mwezi Desemba mwaka huu. Hafla hiyo ya kila mwaka ya kitamaduni inalenga, miongoni mwa mengine, kudhihirisha na kukuza umoja wa Jamii ya Waluo. Pia inalenga kuonesha urathi wa kitamaduni wa Waluo kwa kizazi kipya wakati huu ambapo mabadiliko ya kitamaduni yanayoshawishiwa na mtindo wa maisha yakishuhudiwa. Makala ya mwaka huu yatafanyika chini ya kauli mbiu: "Kusherehekea Mageuzi na Mabadiliko ya Utamaduni wa Waluo."
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive