368 views
3 months ago General
Mahakama Kuu imeongeza muda wa kutekeleza maagizo yaliyotolewa siku ya Alhamisi ya kusimamisha kuanzishwa kwa kituo cha karantini cha wagonjwa wa Ebola humu nchini. Jaji Patricia Nyaundi ameamuru serikali kutoa taarifa kamili kuhusu kituo hicho cha karantini. Hii ni baada ya Taasisi ya Katiba kuifahamisha mahakama kwamba, walizuiwa kuingia katika eneo la karantini la Laikipia. Haya yanajiri huku mtu mmoja akiaga dunia kutokana na majeraha wakati wa maandamano ya kupinga ujenzi wa kituo hicho , yaliofanyika siku ya jumatatu mjini Nanyuki.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive