10 views
1 month ago General
Mahakama Kuu imewaagiza watoaji huduma za mikopo kuanza mchakato wa kuwasilisha madai yao katika shughuli zinaoendelea za kufunga Kampuni ya Bima ya United Limited kufikia tarehe 11 mwezi wa tisa mwaka huu. Mzozo huo, ambao umechukua takriban miaka 18, umezuka tena baada ya wahudumu wa mikopo kuwasilisha ombi la kumfurusha mfuatiliaji wa deni Kamal Anantroy Bhatt, wakimshutumu kwa kutumia shilingi milioni 151.8 kutoka kwa mali ya kampuni hiyo bila idhini. Hata hivyo, Bhatt anaomba shilingi laki nne unusu za Kenya ili kuchapisha taarifa rasmi katika magazeti ya humu nchini ili kuwawezesha wahudumu wa mikopo kuwasilisha ushahidi wa madeni yao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive