17 views
4 months ago General
Rais William Ruto amesema kuwa serikali imepata ufanisi mkubwa katika kuleta uthabiti kwenye sekta ya elimu humu nchini. Akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 120 tangu kuanzishwa kwa shule ya Maseno katika kaunti ya Kisumu, Ruto alsiema kuwa mashauriano na wadau wa elimu yamefanikisha kulainishwa kwa marekebisho ya mtaala nchuini na hivyo kuleta uthbiti katika mpango wa elimu na mafunzo ya umilisi. Na kuhusiana na uhaba wa walimu na muundo msingi shuleni rais alisema kuwa serikali yake imepiga hatua kubwa katika kushughulikia mapengo hayo na kwamba serikali yake kufikia sasa imewaajiri walimu elfu-10 na kujenga madarasa elfu-23 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anatuarifu zaidi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive