10 views
1 week ago
Halmashauri ya kukabiliana na bidhaa ghushi humu nchini imetangaza kanuni zinanopaniwa kudhibiti uuzaji wa pombe haramu. Akiongea mjini Naivasha, mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyoDkt. Robi King’a alisema miongoni mwa hatua hizo ni kuanzishwa kwa nembo ya utambuzi ya kila aina ya kileo inayouzwa humu nchini ambayo itapambanua bidhaa halisi kutoka zile bandia. Dkt. King'a amesema halmashauri hiyo imeanzisha kampeni mahsusi ya uhamasisho kwa wateja na akawataka watengenezaji bidhaa hizo kuhakikisha vileo wanavyouza vinafiki viwango vya ubora.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive