3 views
1 week ago
Mashirika ya ajira kutoka maeneo ya Mashariki na Pembe ya Afrika yameanza mipango ya kubuni shirikisho la kikanda kwa lengo la kukuza taratibu za haki na adilifu za uajiri na kuwalinda wafanyakazi wahamiaji. Shirikisho lililopendekezwa litayaleta pamoja mashirika ya kibinafsi ya ajira kutokaKenya, Ethiopia, Tanzania, Uganda, Somalia, Sudan Kusini miongoni mwa mataifa mengine ya kanda hii ili kuimarisha ubia katika utoaji nafasi za ajira na ulinzi wa wanaotafuta kazi nje hususan katika eneo la Mashariki ya Kati. Akihutubia kikao cha wawakilishi wa mashirika hayo mjini Mombasa, Mshauri Mkuu wa Kiufundi kuhusu ajira ugenini katika Shirikisho la Kimataifa la Leba Aida Awel alisema shirikisho lililopendekezwa litatoa nafasi kwa mashirika ya ajira kushughulikia changamoto za wafanyakazi wahamiaji mbali na kuinua viwango vya kazi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive