9 views
1 week ago General
Wadau muhimu katika mfumo wa uchaguzi wameibua tahadhari kuhusiana na ongezeko la visa vya ghasia za kisiasa vinavyoshuhudiwa kote nchini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka-2027. Wakizungumza wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu usalama na tume ya uchaguzi na mipaka nchini-IEBC jijini Nairobi, wadau walionya kuwa mtindo wa kuogofya ulioripotiwa kwenye kaunti za Homa Bay, Nakuru, Bomet, na Migori unasheheni mitindo sawa na ile iliyojiri kabla ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka-2007/2008. Na kama mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anavyoarifu, mwenyekiti wa tume ya IEBC Erastus Ethekon sasa amesema yamkini maafisa laki mbili wanapokea mafunzo maalum kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive