5 views
1 week ago General
Makala ya 123 ya maonesho ya kimataifa ya Mombasa yalianza Mombasa huku miito ikitolewa kwa wakulima kuthamini matumizi ya teknolojia pamoja na kuanza kilimo cha kisasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Akifungua maonesho hayo ya siku tano kuhusu kilimo, mwenyekiti wa chama wa kilimo nchini John Kibira, alisisitiza uwepo wa chakula cha kutosha nchini unakabiliwa na changamoto kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotabirika na akaongeza kuwa ni lazima wakulima wabuni mbinu zinazofaa za kilimo ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha nchini. Maonesho hayo yanayoandaliwa kila mwaka yanawaleta pamoja wakulima, wajasiriamali, mashirika ya serikali pamoja na wataalamu wa viwanda ili kuonesha ubunifu wao unaonuiwa kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo pamoja na kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive