205 views
3 weeks ago General
Baadhi ya wazee kutoka eneo la Mlima Kenya Mashariki wamemuidhinisha naibu rais Kithure Kindiki kuwa mgombea mwenza wa rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wakizungumza wakati wa mkutano maalum wa mabaraza ya wazee wa jamii za wakazi wa Mlima Kenya Mashariki katika kaunti ya Embu, wazee hao vile vile walitoa wito kwa wenzao katika eneo la Mlima Kenya Magharibi kuwaunga mkono jinsi wamekuwa wakiwaunga mkono kisiasa kwa miongo kadhaa kwa kumuunga mkono rais William Ruto na naibu wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka-2027.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive